Tuesday 1 January 2013

Kesi ya Lulu yatinga Mahakama Kuu



Msanii wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael (Lulu)


Kesi  ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii Elizabert Michael maarufu kama Lulu, (pichani) imesajiliwa kwa namba 125/2012 katika Mahakama Kuu, Tanzania.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari ndani ya mahakama hiyo, kesi hiyo kwa sasa inasubiri kupangiwa kwa hakimu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Aidha,chanzo hicho kimeeleza kuwa, hati ya dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo tayari imewasilishwa mahakamani hapo.
Wiki iliyopita, katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama, Agustina Mmbando, ilielezwa kuwa mashahidi upande wa mashitaka watakuwa tisa.

Mashahidi ni pamoja na aliyekuwa daktari wa marehemu, Paplas Kagaige, mdogo wake marehemu,  Seki Bosco na mama mwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, Sofia Kasimu.

Wengine ni askari polisi wa kituo cha Oysterbay Ester Zephania na Ofisa wa Polisi ofisi ya Mkuu wa Upelelezi kituoni hapo, Daniel Shila pamoja na mwanafunzi Doris ambaye ni rafiki wa mshtakiwa.

Wengine ni Daktari Magreth mkazi wa Tabata Kimanga ambaye alisimamia uchunguzi wa awali wa mwili wa marehemu uliofanyika Muhimbili chini ya jopo la madaktari, Afisa Uhamiaji Ispekta Mweisiga ambaye aliteuliwa na kamati ya maandalizi ya msiba wa Kanumba kwenda Muhimbili kutambua mwili wa marehemu.

Mashahidi wengine ni askari Renatus wa Oysterbay aliyeandika maelezo ya mshtakiwa.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 11, mwaka huu akikabiliwa na tuhuma za mauaji ya Kanumba yaliyotokea Aprili 7, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment