Spika awafunga wabunge midomo.
SAKATA la ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka
Mtwara hadi Dar es Salaam, linaendelea kuwa utata mtupu kwa Serikali ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na usiri uliotanda mradi huo.
Rasilimali hiyo imezua vurugu kubwa mkoani Mtwara hivi karibuni na
kusababisha vifo vya watu kadhaa pamoja na uharibifu wa mali za serikali
na viongozi wa kisiasa, huku wananchi wakitaka waelezwe jinsi
watakavyonufaika.
Hata hivyo, utata mkubwa umenza kujitokeza katika suala hilo kutokana
na wawekezaji wa mradi huo kutishia kujitoa endapo mgogoro huo
usipopatiwa ufumbuzi haraka.
Tanzania Daima Jumatano limedokezwa kuwa, kutokamilika kwa sera ya
gesi ni sababu mojawapo inayochangia kukuza mgogoro huo kwani hadi sasa
haijulikani nani...