Jeshi la Polisi ZNZ linawashikilia
watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na shambulizi la risasi dhidi ya
Padri Amros Nkenda(52), mwishoni mwa wiki iliyopita.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi
ZNZ Inspekta Mohammed Mhina, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa usiku wa
kuamkia leo kwa ushirikiano wa Makachero wa Polisi ZNZ na wenzao kutoka
PHQ Dsm.
Bila ya kuwataja majina kwa kuhofia
kuingilia upelelezi wa kuwapata wengine, Inspekta Mhina amesema
watuhumiwa hao wanaendeleo kuhojiwa ili kuwapata washiriki wote
waliohusika ktk njama za kumvamia na kumshambulia kwa risasi Paroko wa
Parokia ya Mpendae mjini ZNZ.
Amesema
bado Makachero hao wa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Jana akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Naibu DCI ZNZ,
ACP Yusuf Ilembo, amesema Polisi watahakikisha wale wote waliohusika ktk
shambulizi hilo wanatiwa nguvuni na kukabili mkono wa sheria. Mwisho.
0 comments:
Post a Comment