Monday, 28 January 2013

LULU APATA DHAMANA

 
 
Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la kisanii kama Lulu, sasa anaweza kupata dhamana kutoka Mahakama Kuu juu ya kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake.
Taarifa kutoka TAJOA inasema..... Mahakama kuu kanda ya Dar Es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inadhaminika. Kwa maana hiyo, Lulu sasa anaweza kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya 2013 akiwa na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.
Taarifa hii imetoka kwa muungano wa waandishi wa habari Tanzania TAJOA.